Klabu
kongwe na pendwa zaidi duniani, Manchester United imekamilisha
makubaliano yao binafsi na mshambuliaji wake mpya Mkolombia, Radamel
Falcaohave ikiwa ni mazingira ya kuhakikisha hakutatokea mgogoro wowote
baadaye endapo wataamua kumpa Falcao mkataba wa kudumu Old Trafford.
Falcao ni mmoja wa wanandinga wenye rekodi ya majeraha ya mara kwa mara |
Falcao
28, ametua kunako Manchester United kwa ada ya mkopo ya pauni milioni 6
kutoka FC Monaco ya Ufaransa saa chache kabla ya dirisha kubwa la
usajili kufungwa July Mosi, 2014.
Kwa
mujibu wa katibu mkuu mtendaji wa Manchester United , Ed Woodward
alisema, mpaka sasa wameshakubaliana na FC Monaco kulipa kiasi cha Pauni
milioni 43.5 endapo watakubali kumpa Falcao mkataba wa kudumu klabuni
hapo baada ya msimu huu wa ligi kuu Uingereza kumalizika na hakutatokea
madiliko yoyote ya kiwango hicho cha pesa.
Manchester
United, wameamua kuweka sawa mambo hayo haraka ili kuzuia purukushani
iliyowakuta 2009 baada ya kumsajili kwa mkopo mshambuliaji CarlosTevez
kutoka West Ham United na baadaye kukubali kubaki naye kwa ada ya
uhamisho ya Pauni milioni 25, lakini dili hilo likabuma kwa kuwa Tevez
hawakuridhiani maridhiano binafsi na Man U (personal terms) ambapo
aliamua kutimukia kwa mahisumu wao wa jadi Manchester City.
Kwa
sasa Falcao anatumikia Mashetani Wekundu kwa makubaliano ya kutafuna
kitita cha pauni milioni 250,000 kwa wiki mbali na marupurupu
yanayotokana na haki za matangazo.
0 comments:
Post a Comment