KIUNGO
Shinji Kagawa amerejea kwa kishindo Bundesliga baada ya mchezaji huyo
wa zamani wa Manchester United kufunga bao na kutoa pasi katika ushindi
wa 3-1 wa Borussia Dortmund dhidi ya Freburg akicheza mechi ya pili
tangu arudi 'nyumbani'.
Mwanasoka
huyo wa kimataifa wa Japan alimsetia Adrian Ramos kufunga bao la kwanza
dakika ya 34, kabla ya yeye mwenyewe la pili kana ya mapumziko.
Kagawa
alipata mapokezi mazuri akirejea Wesfalenstadion, ambako mashabiki
walibeba mabango na bendera zenye picha yake na kumshangilia ile mbaya
wakiimba jina lake.
Aliondoka
Dortmund kuhamia United mwaka 2012, lakini akashindwa kung'ara na
kuwashawishi makocha wa timu hiyo kumpa nafasi ya kudumu kwenye kikosi
cha kwanza Old Traffford baada ya kusajiliwa kwa Pauni Milioni 12.
Nyota
huyo mwenye umri wa miaka 25 msimu ameuzwa na kocha Louis van Gaal kwa
dau la hasara la Pauni Milioni 6.3 akiungana tena na kocha Jurgen Klopp,
ambaye alisema alitamani kumwaga machozi namna mchezaji huyo alivyokuwa
anagfanyiwa United.
Dortmund tayari imeuaza jezi 5,000 za Kagawa baada ya kiungo huyo kurejea klabuni.
Shinji Kagawa akitafita mbinu za kumtoka Julian Schuster
Shabiki akiwa amebeba bang la picha ya Shinji Kagawa
0 comments:
Post a Comment