KIUNGO
wa Chelsea Cesc Fabregas ameweka historia katika Ligi Kuu ya England
baada ya kuibuka mchezaji wa kwanza kutoa pasi za mabao katika mechi
sita mfululizo.
Huo
ni mwendelezo wa tangu akiwa Arsenal, ambako alitoa pasi za mabao
katika mechi zake mbili kubwa za mwisho kabla ya kuondoka The Gunners
kurejea Barcelona mwaka 2011.
Fabregas
amevunja rekodi kwa pasi mbili za mabao kwa Diego Costa kwenye ushindi
wa The Blues wa 4-2 dhidi ya Swansea ambao unawaweka kileleni mwa Ligi
Kuu England.
Fabregas akizozana na mchezaji mwenzake Diego Costa
Pia
alimsetia Costa mabao aliyofunga dhidi ya Everton na Hazard dhidi ya
Leicester akithibitisha kocha wa Chelsea Jose Mourinho hakukosea
kumnunua.
Kiungo
huyo wa kimataifa wa Hispania alinza na moto wake katika urejeo wake
England akiseti mabao ya Andre Schurrle na Branislav Ivanovic katika
wiki ya kwanza ya msimu na Burnley.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27, baada ya kung'ara Arsenal sasa anafanya vita pia Magharibi mwa London.
Fabregas
alimsetia Robin van Persie kufunga wakifungwa na Bolton baada ya kutoka
kumsetia Theo Walcott na van Persie katika sare ya 3-3 na wapinzani wao
wa Kaskazini mwa London, Spurs.
Kabla
ya mechi na Swans, Fabregas alikuwa miongoni mwa wachezaji sita
waliotoa pasi za mabao katika mechi tano mfululizo walizocheza Ligi Kuu
ya England.
Lakini
shujaa huyo mpya wa Chelsea, sasa anawapiku Darren Anderton, Gianfranco
Zola, Ryan Giggs, Thierry Henry na Antonio Valencia kwenye chati ya
vinara wa kutoa pasi za mabao.
0 comments:
Post a Comment