Anatua Bernabeu: Mchezaji wa Colombia
aliyeng`ara kombe la dunia na kutwaa tuzo ya mfungaji bora, James
Rodriguez anatarajia kujiunga na Real Madrid jumatano.
Imechapishwa Julai 21, 2014, saa 5:56 asubuhi
NYOTA wa kombe la dunia, James
Rodriguez, jumatano ya wiki hii atasaini mkataba na Real Madrid
utakaogharimu ada ya uhamisho ya paundi milioni 60.
Rodriguez alikuwa nchini Hispania jana
jumapili akitokea kwao Colombia na anaelekea katika klabu ya Manaco
ambapo ataaga wiki hii kabla ya kurudi tena mjini Madrid kusaini mkataba
wa miaka sita.
Rais wa Real Madrid , Florentino Perez
yuko Marekani kusini kwa masuala ya kibishara, lakini anarejea wiki hii
kuhakikisha kuwa mabingwa hao wa Ulaya wanatumia zaidi ya paundi milioni
80 kwa kumuongeza Rodriguez baada ya kumsajili Toni Kroos kutoka Bayern Munich wiki iliyopita kwa dau la paundi miliobi 20.
Kijana wa dhahabu: Rodriguez anatarajia kusaini mkataba wa miaka sita wiki hii na miamba ya La Liga.
Endelea hivyo hivyo: Real wanaamini nyota huyo mwenye miaka 21 anaweza kuonesha kiwango chake cha kombe la dunia
Uhamisho mkubwa: Rodriguez alikuwa Hispania akitokea Colombia na anakwenda Monaco kuaga.
Msimu uliopita, mchezaji Gareth Bale
alisajiliwa kwa dau la paundi milioni 85 ambapo Real Madrid walimuuza
Mesut Ozil kwenda Asernal kusaidia kupata hela ya kulipa mkwanja huo.
Usajili huu mwingine mkubwa majira haya
ya kiangazi, unaweza kusababisha angalau mchezaji mmoja au watatu
kuondoka ili kupata hela.
Manchester United wanaiwinda saini ya
Angel Di Maria licha ya msimamo wa kocha Carlo Ancelotti kutaka
Muargentina huyo abaki klabuni hapo.
Kuvunja benki ili kumnunua Rodriguez
kunaweza kuwashawishi zaidi Madrid kumuuza Sami Khedira na kushuka dau
walililotaja la paundi milioni 20.


0 comments:
Post a Comment