Gwiji: Mourinho (kushoto) alimleta Drogba Chelsea mwaka 2004 kutokea klabu ya Marseille.
Imechapishwa Julai 21, 2014, saa 6:35 mchana
NDOTO ya Didier Drogba kurudi tena Chelsea inatarajia kukamilika wiki hii.
Mazungumzo ya kumpa mkataba wa mwaka
mmoja wa ukocha na mshambuliaji wa akiba yamekuwa yakiendelea vizuri na
kuelekea kukamilika na gwiji huyo wa darajani mwenye miaka 36 ataungana
na kocha wake wa zamani, Jose Mourinho.
Inafahamika kuwa Drogba ameshawatumia ujumbe baadhi ya wachezaji wenzake wa zamani wa Chelsea akieleza kuwa anarudi darajani.
Nyota huyo mwenye miaka 36 amezivutia klabu kadhaa nchni Qatar, wakati Juventus wakipambana namna ya kuinasa saini yake.
Chelsea inataka kupunguza wachezaji
wenye umri mkubwa kwenye kikosi chake, lakini inatambua mchango wa
Drogba nje na ndani ya uwanjani.
Wanaamini kuwa uzoefu wa mshambuliaji
huyo utakuwa na ushawishi mkubwa katika benchi la ufundi na atatoa
msaada kwa nyota mpya, Diego Costa.
Chelsea wametumia vizuri majira haya ya
kiangazi na wataendelea kuongeza wachezaji, lakini wamempoteza Samuel
Eto`o na Demba Ba, wakati Romelu lukaku anaweza kujiunga na Everton licha ya awali kuwepo kwa mipango ya kumrudisha.
Kuwa kocha mchezaji kutasaidia kwenda na sheria ya matumizi ya fedha kwasababu mshahara wake utaingia kwenye bajeti ya makocha.
Drogba alisaini kwa mara ya kwanza Chelsea miaka 10 iliyopita na kuondoka mwaka 2012.
Kuthibitisha kuondoka kwake, Drogba
aliiambia tovuti ya klabu kuwa: "Nataka kumaliza tetesi zote na
kuthibitisha kwamba naondoka Chelsea. Yamekuwa maamuzi magumu kwangu
kufanya na ninajivunia kwa kile tulichopata".
"Lakini muda wa changamoto mpya kwangu umefika. Kama sehemu ya timu nimesaidia sana na kushinda kila kombe lililowezekana".
Drogba alipokuwa akiwashukuru mashabiki wa Chelsea katika mchezo wake wa mwisho ndani ya dimba la Stamford Bridge.


0 comments:
Post a Comment