RYAN Giggs anaweza kupata kazi ya kudumu Manchester United baada ya kocha anayetarajia kujiunga na Mashetani wekundu, Louis Van Gaal kuweka wazi kuwa huwa anapenda kumuacha kocha mmoja aliyekuwa katika kikosi chake kipya kabla ya kujiunga na kuanza kazi rasmi
Giggs alishuhudia timu yake ikimaliza mechi ya mwisho kwa sare ya 1-1 na Southampton jana.
Sasa
kinachosubiriwa ni kuona nini Van Gaal ataamua kuhusu hatima ya Giggs
mara atakapothibitishwa kuwa kocha wa United baadaye wiki hii.
Lakini
kutokana na falsafa ya Mholanzi huyo kubakisha moja ya makocha
waliokuwepo imetoa matumaini kwa Giggs kupata ajira ya kudumu.

0 comments:
Post a Comment