
Awali mechi hiyo tulipanga
ichezwe Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya kwa nia ya kuhakikisha mikoa yote
ya Tanzania inapata fursa ya kuwa mwenyeji wa mechi za kimataifa.
Ili Uwanja wa Sokoine uweze
kuchezwa mechi za kimataifa za mashindano, Shirikisho la Mpira wa Miguu
Afrika (CAF) lilituma Mkaguzi (inspector) wake kwenye uwanja huo
Jumamosi (Mei 10 mwaka huu) ambapo imeamua kuwa marekebisho
yanayofanyika hayatamalizika katika muda stahili, hivyo mchezo huo
kutochezwa Sokoine.
Tunatoa mwito kwa wamiliki wote
wa viwanja kuwasiliana na TFF ili Idara ya Ufundi iwaelekeze maboresho
ya kufanya ili viwanja vingi iwezekanavyo viweze kukidhi viwango
vinavyotakiwa na CAF na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu
(FIFA).
Taifa Stars ambayo ilikuwa kambini mkoani Mbeya itarejea Dar es Salaam keshokutwa (Mei 14 mwaka huu) kujiandaa kwa mechi hiyo.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
0 comments:
Post a Comment