Nyota: Bosi wa Chelsea, Jose Mourinho akimpa zawadia Eden Hazard baada ya kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka
Kipenzi cha mashabiki: Hazard aliifungia Chelsea mabao 14 katika michezo ya ligi na kumaliza katika nafasi ya tatu.
EDEN Hazard amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa Chelsea katika msimu wake wa pili klabuni hapo.
Kiungo
huyo wa kimataifa wa Ubelgiji amefurahia mafanikio ya msimu huu chini
ya kocha Jose Mourinho na kufanikiwa kufunga mabao 14 katika michezo
yote ya ligi kuu na kumaliza akiwa mfungaji bora wa klabu.
Hazard
aliyejiunga na Chelsea majira ya kiangazi mwaka 2012 akitokea klabu ya
Lille ya Ufaransa, mwezi uliopita alishinda tuzo ya PFA ya mchezaji bora
kijana wa mwaka na alishika nafasi ya pili nyuma ya Luis Suarez wa
Liverpool katika tuzo ya mwanasoka bora wa mwaka nchini England.
Hazard alisema: ‘Nataka kusema asante sana”
“Wenzangu
watatu waliotajwa walistahili tuzo hii. Tunafahamu tulicheza kwa
ushirikiano, lakini tuzo binafsi wakati fulani ni nzuri, kwahiyo
nitaichukua tuzo hii mpaka nyumbani kwangu na kufurahia pamoja na
familia yangu”
0 comments:
Post a Comment