KOCHA Luis van Gaal anajiandaa kumchukua Patrick Kluivert akawe msaidizi wake atakapojiunga na Manchester United.
Kwa mujibu wa gazeti la De Telegraaf na Uholanzi, ambalo lina ukaribu na kambi ya Van Gaal, kocha huyo tayari amejihakikishia kazi Old Trafford.
BIN ZUBEIRY inafahamu ulifanyika mkutano siku chache zilizopita baina ya wawakilishi wa Van Gaal na United.
Makocha wapya Old Trafford? Louis van Gaal atamchukua Patrick Kluivert akawe Msaidizi wake Man United
Gwiji: Kluivert alikuwa mchezaji wa Van Gaal katika klabu za Ajax na Barcelona
United
imekanusha madai ya kufikia makubaliano, lakini gazeti pia limesema
Kluivert - kwa sasa anafanya kazi chini ya Van Gaal katika timu ya taifa
ya Uholanzi- anaweza kurithi mikoba iwapo Van Gaal ataondoka.
Mshambuliaji
huyo wa zamani wa kimataifa wa Uholanzi alicheza chini ya Van Gaal
katika klabu za Ajax na Barcelona kabla ya kusajiliwa na Newcastle mwaka
2004.
Kocha
wa makipa, Frans Hoek na mchua misuli, Jos van Dijk pia wanatajwa
kuwamo katika timu ya Van Gaal ya benchi la Ufundi atakayohamia nayo
United.
0 comments:
Post a Comment