Searching...
Thursday, March 20, 2014

VAN PERSIE AINUSURU MAN UNITED


Robin van Persie akishangilia moja ya bao alilofunga usiku wa kuamkia leo walipokuwa wakicheza na Olympiakos katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Robin van Persie alifunga mabao matatu na kuisaidia mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Uingereza Manchester United, kujikatia tiketi ya kushiriki robo fainali ya kombe la klabu bingwa barani Ulaya baada ya kuinyuka Olympiakos mabao 3-0 katika mechi ya mkondo wa pili iliyochezwa Old Trafford.
Van Persie alifunga mkwaju wa penalti baada ya kuchezewa vibaya mda mchache tu kabla ya kumalizika kwa kipindi cha kwanza.
Van Persie akishangilia na Rooney.
Baadaye mshambulizi huyo wa Uholanzi aliongeza bao lingine baada ya kupata pasi nzuri kutoka kwa mshambulizi mwenza Wayne Rooney.
Van Persie alifunga bao lake la tatu kwa mkwaju wa free kick na kumhakikishia Moyes fursa ya kujiunga na Chelsea katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo yenye kitita kikubwa zaidi barani Uropa.
Licha ya mashambulizi kadhaa Olympiacos kutoka Ugiriki mlinda lango wa Manchester United David De Gea alilazimika kufanya kazi ya ziada kuinyima klabu hiyo kutoka Ugiriki bao moja tu la ugenini
Olympiacos ilishinda mechi ya kwanza mabao 2-0 na ilihitaji sare ya aina yeyote ama bao moja tu la ugenini ilikufuzu kwa hatua ijayo kutokana na sheria ya bao la ugenini.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!