Zikiwa zimebakia siku kadhaa kabla ya mechi ya West Ham United vs Manchester United wikiendi hii, kocha wa West Ham Sam Allardyce, ametoa historia ya kuvutia kuhusu yeye na David Moyes.
Allardyce
anasema mwaka 1993, wakati akiwa kocha wa timu ya vijana ya Preston,
alienda kumuangalia Moyes akiichezea Dunfermline dhidi ya Falkirk ili
aone uwezo wake kama anafaa kusajiliwa, na alitumwa na kocha mkuu wa
timu ya Preston John Beck.
Na
pamoja Moyes kuonyeshwa kadi nyekundu kwa kushika mpira makusudi katika
kipindi cha kwanza dakika ya 38, Allardyce aliridhishwa na uwezo wake
na akampelekea ripoti nzuri kocha mkuu Beck.
Moyes alipokuwa akiichezea Preston ambayo Allardyce alikuwa kocha msaidizi |
Moyes
hatimaye alihamia Preston, na baada ya mechi 159 mscotish huyo akawa
kocha wa timu hiyo, lakini alikosa nafasi ya kupanda ligi kuu ya England
baada ya kufungwa kwenye play-offs na Everton mnamo 2002.
Kuelekea
mchezo ambao utawakutanisha Allardyce na Moyes wakati United
itakapoifuata West Ham Upton Park, kocha wa West Ham anakumbuka
alivyomuona Moyes mara ya kwanza.
Allardyce
alisema: 'Alitolewa kwa kadi nyekundu baada ya dakika ya 38 za mchezo.
Niliendesha gari mpaka Scotland, John Beck alinituma nikamtazame.
'Lakini ndani ya hizo dakika 38 nilijua kwamba angefaa kuitumikia Preston."
0 comments:
Post a Comment