Mshambuliaji
Lionel Messi jana alivunja rekodi na kuweka rekodi mpya ndani ya klabu
ya FC Barcelona baada ya kufunga mabao matatu katika mchezo wa ushindi
wa mabao 7-0 dhidi ya Osasuna.
Messi
kwanza alimfikia Paulinho Alcantara kwa kufikisha mabao 369, rekodi
ambayo imekaa kwa takribani miaka 80, Paulinho alifunga mabao 142 katika
mechi za mashindano - 227 katika mechi za kirafiki. Aliichezea Barca
kutoka 1912 mpaka 1927, hata Alcantara aliumia na hakucheza misimu
miwili katika kipindi chote.
Messi
baada ya kuifikia rekodi hiyo, akaongeza mabao mawili na kuweka rekodi
mpya ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa klabu hiyo katika mechi zote
akifikisha mabao 371 - mabao 344 amefunga katika mechi za mashindano, 27
katika mechi za kirafiki.
0 comments:
Post a Comment