Searching...
Friday, December 14, 2012

JUMANNE NENDA JELA MIAKA 30 UACHE UBAKAJI

Mahakama ya Wilaya Kongwa Jana ilimuhukumu Bw. Jumanne Hassan Miaka (22) mkazi wa kijiji cha Liganga, Kata ya Chitego tarafa ya Nzoisa wilayani humo kutumikia kifungo cha miaka (30 ) jela na kuchapwa viboko (12) baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kubaka mwanafunzi wa darasa la tano.
Mwandesha mashtaka, Mkaguzi Wa Polisi  Maulid Manu aliiambia Mahakama hiyo kuwa Bw. Jumanne Hassan alimbaka binti mwenye umri wa miaka (12) ambaye jina lake limehifadhiwa na ni mwanafunzi wa darasa la tano katika shule ya msingi Liganga iliyopo wilayani kongwa.
Mwendesha mashtaka huyo wa Polisi, aliieleza mahakama kwamba Bw. Jumanne Hassan alitenda kosa hilo kwa kumvizia binti huyo aliyekuwa anatoka kununua mahitaji ya dukani alipokuwa ametumwa kisha kumkamata mkono na kumvutia katika chumba cha rafiki yake kilichokuwa jirani na eneo hilo kisha kumbaka na kumtishia kwamba akipiga kelele atamuua.
Alieleza hayo mbele ya mbele ya hakimu wa mahakama ya Wilaya ya Kongwa Bw. Godfrey Pius, aidha alisema tukio hilo lilitokea Novemba moja, mwaka jana (2011) majira ya sa mbili na nusu usiku katika eneo la kijiji cha Liganga, Kata ya Chitego na Tarafa ya Nzoisa Wilayani Kongwa.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!