Searching...
Thursday, December 6, 2012

DK HARRISON MWAKYEMBE NI NOUMER AISEE, ADAKA WATUMISHI WATANO WA MAMLAKA YA BANDARI TANZANIA(TPA)WAKITAKA KUVUSHA MALORI 26 KINYEMELA BANDARINI...!!!


Mtumishi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Gladness Mangelele akitoa maelezo mbele ya Waziri Dk. Mwakyembe baada ya kuhusishwa katika sakata hilo ambapo alidai alikuwa hajui chochote kwani alikuwa  akitekeleza majukumu yake ya kawaida katika idara yake.

Dk. Mwakyembe akikagua Malori yanayodaiwa kutaka kutolewa kinyemela na kampuni ya Dhandho, Malori matano kati ya 26 yalipewa baraka na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) yatolewe.

Marystella Minja akitoa maelezo yake mbele ya Waziri Dk Harrison Mwakyembe baada ya kutuhumiwa katika sakata hilo.

Mmoja wa wafanyakazi wa Mamlaka ya Bandari (TPA) Andrew Masaga (kulia) anayedaiwa kuhusika kula njama ya kutoa malori hayo  akijitetea mbele ya Waziri (hayupo pichani) katika sakata hilo jana jinoni. Kushoto  ni Mkuu wa Polisi Bandarini Afande FM Misilimu

Ofisa Utawala wa kampuni ya Dhandho Antipasi Otieno (kulia) akitoa maelezo mbele ya waziri Dk. Harrison Mwakyembe
Waziri wa Uchukuzi Dk. Harisson Mwakyembe akizungumza na waadishi wa habari Bandarini jijini Dar es salaam Jana  jioni wakati akitoa taarifa ya kukamatwa kwa watumishi wa Bandari wanaodaiwa kutaka kutoa  malori 26 kinyemela  bandarini, watu watano wamekamatwa katika sakata hilo.
 
Dk. Harrison Mwakyembe akiongea na maafisa mbalimbali wa Polisi na Bandari baada ya kukagua magari hayo yaliyotaka kutolewa kinyemela bandarini hapo.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!