Searching...
Friday, October 5, 2012

Washiriki wa Kijiji cha Maisha Plus waingia katika Kijiji chao rasmi Kambini

 Mmoja wa wageni rasmi katika uzinduzi wa kijiji cha Maisha Plus Naibu Waziri wa Jinsia, Wanawake na Watoto Mhe. Ummy Mwalim  akitoa hotuba wakati wa uzinduzi wa shindano hilo kwenye kijiji cha Maisha Plus.
 
 
Washiriki wa mpango wa mama shujaaa wa chakula unaodhaminiwa na benki ya NMB hatimaye wameingia katika kijiji cha Maisha Plus. 

NMB inaamini udhamini huo ni sahihi kutokana na kuwa utakuza kilimo na kuwasaidia wakulima wadogo katika maisha, mapambano dhidi ya njaa,umasikini na uhaba wa ajira miongoni mwa wanawake. 

Vilevile, NMB kupitia mpango wa NMB Financial Fitness unaolenga kuongeza uelewa wa matumizi mazuri ya fedha itapata fursa ya kuwaelimisha washiriki kuhusu huduma za kifedha, uwekaji akiba, kupanga matumizi, matumizi mazuri ya kifedha na mengine mengi.
 Washiriki wa shindano la Maisha plus wakifuatilia uzunduzi huo huku wakiburudika kwa kinywaji cha dafu.
 Naibu Waziri wa Jinsia, Wanawake na Watoto Mhe. Ummy Mwalim (kushoto) na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa Oxfam Bi. Monica Gorman wakifurahia kinywaji cha dafu wakati wa uzinduzi huo.
 Mkurugenzi wa Shindano la Maisha Plus Bw. Masoud A. Kipanya (kushoto) akijadili jambo na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa NMB, Bw. Imani Kajula (kati) pamoja na wageni waalikwa katika uzinduzi huo.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Oxfam Bi. Monica Gorman (kushoto) akiteta jambo na Naibu Waziri wa Jinsia, Wanawake na Watoto Mhe. Ummy Mwalim (kushoto) pamoja na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa NMB, Bw. Imani Kajula.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!