Waziri wa Elimu nchini Kenya Prof Sam Ongeri
Kutafuta njia za kumhakikishia kila mmoja elimu ndiyo ajenda kuu inayozungumziwa kwenye mkutano wa baraza la kiuchumi na kijamii la UM unaondelea mjini Geneva. Zaidi ya wajumbe 500 wanaowakilisha serikali , wafadhili , mashirika ya umma, sekta za kibinafsi na wasomi watajadili na kutoa mapendekezo jinsi dunia wakati huu wa hali mbaya ya uchumi inaweza kutimiza lengo la elimu kwa wote na kuhakikisha malengo ya milenia yametimizwa.
Akiongea kwenye mkutano unaozungumzia changamoto za elimu zinazolikumba bara la Afrika waziri wa elimu nchini Kenya Prof Sam Ongeri amesema kuwa Afrika imeonyesha kupiga hatua kwenye masuala ya elimu tangu mwaka 2000 lakini akasema kuwa kuna changamoto za kupata viwango vinavyohitajika vya elimu.
0 comments:
Post a Comment