Searching...
Thursday, July 7, 2011

Serikali ya Tanzania yakiri kuweko uhaba wa katiba ya Jamhuri ya Muungano

 Serikali ya Tanzania imekiri kuwa, kuna uhaba mkubwa wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwamba, wananchi wengi hawana na hawajui ni wapi wanaweza kuipata katiba hiyo. Hayo yamesemwa na Bi Celina Kombani Waziri wa Katiba na Sheria, ambaye amebainisha kwamba, uhaba wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 umeifanya serikali kufikiria uwezekano wa kuongeza idadi ya maduka ya kuuza nakala za sheria mbalimbali ikiwemo katiba. Waziri wa Katiba na Sheria wa Tanzania amesema kwamba, serikali inajitahidi kwa kadri ya uwezo wake wa kifedha kusogeza huduma kuhusu elimu ya katiba karibu na wananchi, ili kumwezesha mwananchi wa kawaida kupata nakala ya katiba ya sasa. Hata hivyo, alisema Watanzania wengi hivi sasa wanafahamu umuhimu wa kuwa na katiba na sheria za nchi katika maisha yao ya kila siku, kuliko wakati wowote katika historia ya Tanzania. Kuhusu kauli ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda ya kuzindua katiba ifikapo Aprili 26, mwaka 2014, Waziri Kombani amesema, kauli hiyo iko pale pale na haiwezi kubadilika, kwani mchakato wa katiba unakwenda vizuri, hivyo serikali inaamini kuwa ifikapo kipindi hicho katiba itazinduliwa na kuanza kutumika rasmi.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!