Searching...
Saturday, July 30, 2011

Mashambulizi yaliyotokea nchini Norway ni "msiba wa taifa"

Waziri Mkuu wa Norway Bw Jens Stoltenberg amesema mashambulizi yalitokea nchini humo ambayo yamesababisha vifo vya karibu watu 91 ni msiba wa taifa, ambao ni mkubwa kutokea baada ya vita ya pili ya dunia.
Polisi wa Norway wamesema idadi ya vifo kwenye shambulizi la ufyatuaji risasi lililotokea kwenye kisiwa cha Utoeva imeongezeka na kufikia 84, na mlipuko uliotokea mjini Oslo umesababisha vifo vya watu 7.
Habari zinasema mtu mmoja aliyekuwa amevaa sare ya polisi na aliyekuwa na kitambulisho cha polisi alikwenda kwenye kisiwa kimoja kidogo na kuanza kuwapiga watu risasi, saa mbili baada ya mlipuko kutokea katika jengo la serikali mjini Oslo

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!