Searching...
Saturday, July 30, 2011

Shamsi Vuai Nahodha: Vitambulisho vya taifa kuanza kutolewa mwaka huu

Serikali ya Tanzania imesema kuwa, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa inatarajia kuanza kutoa vitambulisho vya taifa kwa awamu ya kwanza mwishoni mwa mwaka huu. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi wa Tanzania Shamsi Vuai Nahodha, amebainisha hayo bungeni wakati akiwasilisha hotuba ya bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2011/2012. Waziri Nahodha amesema kuwa, katika awamu ya kwanza, mamlaka husika itawapatia vitambulisho wafanyakazi wa serikali, wanafunzi wa vyuo pamoja na wafanyabiashara. Aidha amesema kwamba, Watanzania kati ya milioni 25 na 26 wenye umri kuanzia miaka 18, wanatarajia kupatiwa vitambulisho hivyo. Kwa mujibu wa Shamsi Vuai Nahodha kampuni iliyoshinda zabuni ya kutengeneza vitambulisho hivyo ni Iris Corporation Behard kutoka Malaysia na kwamba serikali ilitiliana saini mkataba na kampuni hiyo Aprili 21. Mradi huo utagharimu sh bilioni 355 mpaka kumalizika kwake katika kipindi cha miaka mitano.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!