Searching...
Wednesday, June 29, 2011

Waafrika watuma msafara wa misaada kwa wananchi wa Ghaza



Msafara wa kwanza wa misaada ya kibinaadamu wa Waafrika umeanza safari kuelekea Ghaza kwa ajili ya kuwafikishia misaada wananchi madhlumu wa Palestina waliozingirwa kila upande na utawala dhalimu wa Kizayuni.
Msafara huo wa makumi ya magari una misaada ya dharura kama vile vifaa vya tiba, madawa, mahitaji mengine ya awali, maziwa ya mgando, majenereta na vifaa vya ujenzi vinavyoweza kujenga nyumba 10.
Msafara huo wenye wanaharakati 21 umeanza safari yake kutokea Durban Afrika Kusini na unatarajiwa kufika Ghaza mwishoni mwa mwezi ujao wa Julai.
Magari yote yaliyomo kwenye msafara huo yatatolewa wakfu kwa Manispaa ya Ghaza.
Msafara huo unatarajiwa kupitia Zimbabwe, Zambia, Tanzania, Kenya, Sudan, Misri na baadaye Ghaza.
Hata hivyo tayari maafisa wa Misri wamesema kuwa hawataruhusu msafara huo upitie nchini humo.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!