Searching...
Wednesday, June 29, 2011

Utawala wa Libya wapinga hukumu ya kutiwa mbaroni Gaddafi, Marekani yafurahi


Utawala wa Libya umepinga hukumu ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC ya kutiwa mbaroni kiongozi wa nchi hiyo Muammar Gaddafi.
Msemaji wa utawala wa Libya amenukuliwa akisema kuwa, hatua ya ICC ya kutoa waranti wa kutiwa mbaroni Gaddafi ni katika njama za NATO za kutaka kuendeleza mashambulizi dhidi ya nchi hiyo.
Msemaji huyo amesema pia kuwa, Libya si mwananchi wa ICC hivyo hukumu ya mahakama hiyo haina thamani yoyote kwake.
Itakumbukwa kuwa, jana Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC ilitoa waranti wa kutiwa mbaroni Muammar Gaddafi, mwanawe Seiful Islam na Mkuu wa shirika la Kijasusi la Libya kwa tuhuma za kufanya jinai dhidi ya wapinzani wa Gaddafi.
Wakati huo huo Marekani imesema imefurahishwa sana na uamuzi wa ICC wa kutoa hukumu wa kutiwa mbaroni kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!