Searching...
Wednesday, June 29, 2011

China yatoa kanuni mpya ya kuwasaidia watu wanaotumia dawa za kulevya

Serikali ya China imetoa kanuni mpya inayowataka watu wanaotumia dawa za kulevya nchini humo kujitokeza kwa hiari kusaidiwa ili kuepuka kuadhibiwa.
Kanuni hiyo ikiwa sehemu ya nyongeza ya sheria ya China ya kupambana na dawa za kulevya iliyoanza kutekelezwa miaka mitatu iliyopita, inalenga kuwahamasisha watu wanaotumia dawa za kulevya kushiriki kwa hiari kwenye mpango unaowekwa na serikali wa kuwasaidia waweze kuishi maisha ya kawaida. Kanuni hiyo pia inabainisha haki na wajibu wa watu wanaotumia dawa za kulevya, na kutaka mitaa na familia zichangie kuwasaidia watumiaji wa dawa za kulevya.
Kwa mujibu wa takwimu za hivi punde, mpaka sasa zaidi ya Wachina milioni 2 wameshiriki kwenye mpango wa kuwasaidia watumiaji wa dawa za kulevya.
Kanuni hiyo mpya inatolewa siku chache tu baada ya walimwengu kuadhimisha siku ya kupambana na dawa za kulevya duniani.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!