
Martin Nesirky msemaji wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, maafisa 12 wa kimataifa wa umoja huo wamehamishiwa nchini Tunisia kwa muda kutokana na machafuko nchini humo.
Magenge ya Walibya wenye hasira jana yalishambulia balozi za nchi za Magharibi na Umoja wa Mataifa mjini Tripoli baada ya vikosi vya NATO kushambulia makazi ya familia ya Muammar Gaddafi na kumuua mwana mdogo wa dikteta huyo wa Libya na wajukuu zake watatu. Russia imesema kuwa NATO imevuka mipaka ya makubaliano ya Umoja wa Mataifa ya kuwalinda raia wa Libya kwa kufanya mashambulizi hayo.
0 comments:
Post a Comment