Searching...
Tuesday, May 10, 2011

Katibu mkuu wa NATO asema mgogoro nchini Libya hauwezi kutatuliwa kwa nguvu ya kijeshi tu

Katibu mkuu wa jumuiya ya NATO Bw. Anders Rasmussen tarehe 8 alipohojiwa na shirika la habari la Marekani CNN Marekani alisisitiza kuwa, ingawa kiongozi wa Libya Bw. Moammar Gaddafi hatakuwa na siku nyingi madarakani, lakini mgogoro wa Libya hauwezi kutatuliwa kwa njia ya kijeshi tu.
Bw. Rasmussen amesema kampeni ya kijeshi inayoongozwa na NATO imezuia vitendo vya Bw. Gaddafi na kumfanya akae katika hali ya upweke siku hadi siku, siku yake ya mwisho inakaribia.
Amesema ni lazima kutambua kuwa njia ya kijeshi pekee haiwezi kutatua mgogoro wa Libya, bali njia ya kisiasa inapaswa kutumika katika kutatua mgogoro huo.
Bw. Rasmussen amesisitiza kuwa kampeni ya kijeshi ya NATO haitasimamishwa, ila tu malengo yake matatu yatatimizwa, ambayo ni pamoja na kusimamisha mashambulizi dhidi ya raia, misaada ya kibinadamu iweze kuingia nchini Libya mara moja bila vizuizi, na kulirudisha jeshi la Bw. Gaddafi kwenye kambi yao.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!