Searching...
Tuesday, May 10, 2011

Kifo cha Osama chaendelea kuzusha maswali mengi, DRC yalaani kuuawa kwake

  Waziri wa Habari na Mawasiliano wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Lambert Membe Omalanga amelaani vikali hatua ya Marekani ya kumuua kiongozi wa kundi la kigaidi la Al-Qaeda Osama Bin Laden. Omalanga ambaye pia ni msemaji wa serikali ya Kinshasa amesema kuwa Marekani ilipaswa kumkamata Bin Laden akiwa hai na kumfikisha mbele ya vyombo vya sheria badala ya kumuua. Amesema kwamba kwa hivi sasa hakuna tofauti kati ya Marekani na Osama kwani wote ni wauaji. Huku hayo yakijiri, taarifa zilizotolewa na gazeti la The Nation la Pakistan toleo la jana, zinaeleza kuwa Osama alijilipua kwa bomu na mwili wake kukatikakatika vipande kiasi kwamba ilikuwa vigumu kuutambua na wala hakuuawa kwa kupigwa risasi na makomandoo wa Marekani kama ilivyodaiwa na Rais Barack Obama wa nchi hiyo.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!