Searching...
Sunday, May 8, 2011

Baraza la uchumi duniani latoa ripoti kuhusu nguvu ya ushindani ya Afrika

Baraza la Uchumi la Dunia, Benki ya Maendeleo ya Afrika na Benki ya Dunia tarehe 4 zilitoa Ripoti ya mwaka 2011 kuhusu nguvu ya ushindani ya Afrika zikisema, katika miaka ya hivi karibuni, uchumi wa Afrika umepata mafanikio yanayovutia duniani, lakini ili Afrika iweze kudumisha maendeleo endelevu, nchi mbalimbali barani humo zinapaswa kufanya kazi nyingi zinazotakiwa kufanyika.
Ripoti hiyo imetoa mapendekezo kuhusu mwelekeo wa nchi za Afrika katika pande nne, kwanzi ni lazima kuwa na bidhaa na masoko ya aina mbalimbali; pili, kueneza elimu ya hali ya juu, na kuinua usimamizi wa uwezo wa kiteknolojia, tatu, kuwasaidia wanawake kuanzisha shughuli zao ili kujiendeleza; na nne kuendeleza uchumi wa utalii.
Katika ufunguzi wa mkutano wa Afrika wa Baraza la Uchumi wa Dunia Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini alisema, nchi za Afrika zinapaswa kuzibadilisha nguvu zao za maliasili kuwa uwezo wa kujipatia maendeleo endelevu, na kuanzisha uhusiano wa ushirikiano wa aina mpya wakati zinapokuwa na mawasiliano ya kiuchumi na kibiashara na nchi na sehemu nyingine duniani, ili kutimiza lengo la kunufaishana.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!