Searching...
Monday, January 31, 2011

Waganda kufuata nyayo za Wamisri na Watunisia ili kuleta mabadiliko

 Kiongozi wa upinzani nchini Uganda ameonya kuwa, wananchi wa nchi hiyo huenda wakafuata nyayo za Wamisri na Watunisia kuleta mabadiliko nchini humo endapo uchaguzi ujao wa Februari 18 utatawaliwa na mizengwe, wizi wa kura na uchakachuaji wa matokeo. Taarifa kutoka Uganda zinasema kwamba, Dakta Kizza Besigye ambaye anawania kiti cha urais katika uchaguzi ujao wa Rais akishika bendera ya muungano wa vyama kadhaa vya upinzani amesema kinagaubaga kwamba, wananchi wa Uganda huenda wakafuata nyayo za Wamisri na Watunisia kumuondoa madarakani Rais Museveni endapo uchaguzi ujao haufanyika katika mazingira huru na ya haki. Besigye mgombea wa kiti cha Urais sambamba na kuashiria kwamba, nchini Uganda hakuna Rais ambaye amewahi kukabidhi madarakani kwa amani bali kila Rais wa nchi hiyo alitimuliwa ofisini na ametoa wito wa kufanyika uchaguzi huru na wa haki. Mrengo wa upinzani nchini Uganda mara kwa mara umekuwa ukionyesha wasi wasi wake mkubwa ulionao juu ya zoezi la uchaguzi mkuu ujao na kuituhumu tume ya uchaguzi kwamba, inakipendelea chama tawala cha Rais Museveni cha NRM.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!