Searching...
Monday, January 31, 2011

Asilimia 99 ya wapiga kura wanaunga mkono kujitenga na Sudan



Kwa mujibu wa matokeo ya awali ya kura za maoni yaliyotolewa na tume ya upigaji kura za maoni ya sehemu ya kusini mwa Sudan tarehe 30 kwenye tovuti yake, asilimia 98.83 ya wapiga kura wanaunga mkono kujitenga na Sudan. Serikali ya Sudan imesema itakubali matokeo ya upigaji kura huo. Kwa mujibu wa mpango husika, kama tume hiyo haitapokea malalamiko yoyote, itatangaza matokeo ya mwisho ya upigaji kura huo tarehe 7 Februari, ama sivyo, tume hiyo itafanyia uchunguzi malalamiko hayo na kufanya uamuzi, na kutangaza matokeo ya mwisho tarehe 14 Februari.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!