Searching...
Thursday, January 27, 2011

Familia ya rais wa Misri yatoroka, ghasia zazidi



Mwana wa kiume wa rais Husni Mubarak wa Misri, ambaye anatabiriwa kumrithi, amekimbilia Uingereza akiwa na familia yake huku maandamano dhidi ya serikali yakiendelea.
Kwa mujibu wa Tovuti ya Akhbar al Arab, ndege iliyokuwa imebeba Gamal Mubarak, mke wake na binti yake iliondoka Misri Jumanne na kuelekea London.
Familia ya Mubarak imetoroka huku machafuko na maandmano dhidi ya utawala wa kiimla wa Mubarak yakiendelea katika mji mkuu wa Misri Cairo na miji mingine nchini humo. Maelfu ya wananchi wa Misri wamemiminika mitaani wakitaka mapinduzi kama yake yaliyojiri nchini Tunisia. Waandamanaji wanataka serikali ya Misri ifutilie mbali sheria ya hali ya hatari ambayo imekuwepo kwa muda wa miaka 30 sasa. Aidha wanataka ipitishwe sheria ya kumzuia rais kutawala kwa muda wa zaidi ya mihula miwili. Takwa lingine la waandamanaji ni kumtaka Waziri wa Mambo ya Ndani Habib al Adly ajiuzulu. Waandamanaji Misri pia wanalalamikia hali ngumu ya maisha na ukosefu wa ajira.Hadi sasa watu wanne wameuawa katika machafuko ya Misri yaliyoanza Jumatano. Kati ya waliouawa ni afisa mmoja wa polisi ambaye alishambuliwa na waandamanaji. Waandamanaji Misri wamekaidi amri ya serikali ya kutoandamana na wameapa kuendeleza harakati zao hadi matakwa yao yatekelezwe.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!