Searching...
Thursday, January 27, 2011

Maandamano makubwa ya kuipinga serikali yatokea nchini Misri

Maandamano makubwa ya kuipinga serikali yamefanyika tarehe 25 nchini Misri, ambapo baadhi ya waandamanaji walipambana na polisi, na kusababisha vifo na majeruhi.
Maandamano hayo yalifanyika katika miji ya Cairo, Alexandria na Suez nchini Misri. Huko Cairo, waandamanaji walianza kukusanyika adhuhuri kwenye uwanja wa Ukombozi ulioko katikati ya mji huo, na hadi kufikia usiku idadi ya waandamanaji ilizidi elfu kumi, polisi wengi walilinda utaratibu kwenye uwanja huo. Saa saba usiku wa tarehe 26, polisi walirusha mabomu ya machozi na kuwatawanya waandamanaji.
Maandamano hayo ni makubwa zaidi kutokea nchini Misri katika miaka ya hivi karibuni. Waandamanaji hao wanadai kutoridhishwa na ufisadi wa serikali, kupandwa kwa bei za vitu na ukosefu mkubwa wa ajira.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!