Searching...
Monday, December 27, 2010

Ban Ki-moon alaani vikali shambulizi la bomu la kujiua nchini Pakistan

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa tarehe 25 alitoa taarifa akilaani vikali shambulizi la bomu la kujiua, lililotokea katika sehemu ya Bajaur nchini Pakistan.
Taarifa hiyo ilisema, Bw. Ban Ki-moon alishtushwa na shambulizi hilo la kigaidi lililotokea katika kituo cha ugavi wa chakula cha Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa, kilichopo katika sehemu ya Bajaur, na kulaani vikali kitendo hicho cha kigaidi dhidi ya raia. Pia Bw. Ban Ki-moon alitoa salamu za rambirambi kwa ndugu wa watu waliouawa kwenye shambulizi hilo.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!