Searching...
Monday, December 27, 2010

Familia za Wasomali waliokamatwa Uholanzi wakanusha tuhuma dhidi yao

 Familia za Wasomali 12 waliokamatwa nchini Uholanzi zimekanusha madai yaliyotolewa dhidi ya raia hao kuwa walikuwa wakipanga mikakati ya kuendesha mashambulio ya kigaidi nchini humo. Waendesha mashtaka wa Uholanzi wameeleza kuwa polisi ya nchi hiyo imewatia mbaroni Wasomali 12 wanaoshukiwa kula njama ya kufanya mashambulizi ya kigaidi huko Uholanzi. Taarifa ya waendesha mashtaka hao imeongeza kuwa raia hao 12 wa Kisomali wenye umri kati ya miaka 19 hadi 48 walitiwa mbaroni Ijumaa usiku baada ya shirika la ujasusi na usalama la Uholanzi kutoa taarifa. Wameongeza kuwa, Wasomali kadhaa wanashukiwa kupanga mipango ya kufanya mashambulio ya kigaidi nchini Uholanzi. Hii ni katika hali ambayo, familia na ndugu wa Wasomali hao waliokamatwa wamelalamikia hatua hiyo na kueleza kuwa jamaa zao hao hakuwa na mpango wa kufanya mashambulizi hayo.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!