Searching...
Friday, November 26, 2010

China na Afrika kufungua ukurasa mpya wa ushirikiano wa kirafiki

Balozi wa China nchini Jamhuri ya Congo Bw. Li Shuli tarehe 25 alisema China itashirikiana na watu wa Afrika ili kufungua ukurasa mpya wa ushirikiano wa kirafiki kati ya pande hizo mbili.
Kwenye tafrija ya kusherehekea miaka kumi ya baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika iliyofanywa na ubalozi wa China nchini Jamhuri ya Congo, balozi Li Shuli alisema baraza hilo limekuwa daraja la kuendeleza urafiki wa jadi na jukwaa la kuimarisha ushirikiano halisi kati ya China na Afrika. Kupitia baraza hilo, ushirikiano kati ya China na Jamhuri ya Congo katika mambo ya siasa, uchumi, biashara, utamaduni na elimu unaimarika siku hadi siku.
 
Waziri wa mambo ya nje wa Jamhuri ya Congo alisema katika miaka kumi iliyopita, China imeendelea kushirikiana na Afrika, na ushirikiano huo umekuwa mfano mzuri wa kuigwa kwa nchi zinazoendelea. Jamhuri ya Congo ikiwa ni rafiki wa jadi wa China, itaendelea kuimarisha ushirikiano wa kirafiki na China.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!