Searching...
Friday, November 26, 2010

Luanda-Angola yataka nchi za Afrika zikabiliane na changamoto za usafi na mazingira

Makamu rais wa Angola Bw. Fernando dos Santos tarehe 25 huko Luanda alitoa mwito wa kuzitaka serikali za nchi za Afrika na mashirika ya kimataifa ya Afrika zichukue hatua pamoja, ili kukabiliana na changamoto za mazingira na usafi barani Afrika.
Amesema hayo kwenye ufunguzi w mkutano wa pili wa mawaziri wa masuala ya afya na mazingira katika nchi za Afrika uliofanyika siku hiyo huko Luanda. Bw. Fernando alisema uchafuzi wa mazingira, kelele, ardhi, maji, shughuli za binadamu na njia za kujipatia maendeleo ya uchumi zisizo endelevu zilizochukuliwa na baadhi ya nchi ni chanzo kikubwa cha kuyafanya mazingira ya viumbe yazidi kuwa mabaya barani Afrika. Aidha, alisema asilimia 23 ya watu waliokufa barani Afrika, walikufa kutokana na hatari za mazingira ambazo zinaweza kuepukika, na asilimia 60 ya mazingira ya viumbe imekuwa mabaya au inakabiliwa na shinikizo kubwa la shughuli za binadamu, hivyo serikali za nchi za Afrika zinapaswa kufanya bidii na kuchukua hatua za pamoja katika kulinda mazingira, kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, na kuboresha hali ya usafi.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!