Searching...
Friday, November 26, 2010

UNEP: Malengo ya Maendeleo ya Milenia kutofikiwa kutokana na uhaba wa maji barani Afrika

Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP limesema kuwa malengo ya maendeleo ya milenia huenda yakafeli katika nchi nyingi za Afrika kutokana na uhaba wa maji, vyoo na ukosefu wa usafi wa mazingira. Kwenye ripoti iliyotolewa na UNEP leo hii, mataifa 8 pekee ya barani Afrika ndio yameonyesha dalili za kufikia malengo hayo ya milenia kufikia mwaka wa 2015. Mataifa hayo yametajwa kuwa Algeria, Morocco, Tunisia, Libya, Misri, Afrika Kusini, Angola na Botswana. UNEP imeongeza kuwa, mataifa 26 kati ya 53 ya bara Afrika huenda yakafanikiwa kuyafikia malengo ya milenia katika suala la uwepesi wa kupata maji safi ya kunywa kufikia mwaka wa 2015. Miongoni mwa mambo yaliyopewa kipaumbele wakati wa kubuniwa Malengo ya Maendeleo ya Milenia mwaka wa 2000, ni kukomesha umasikini, kuimarisha elimu, usawa wa jinsia, afya na mazingira.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!