Searching...
Friday, October 1, 2010

Mahakama Kuu ya India yatoa hukumu kuhusiana na msikiti wa Babri

Sample ImageMahakama Kuu ya India imetoa hukumu kuhusiana na eneo lililokuwa likigombaniwa kati ya Wahindu na Waislamu katika mji wa Ayodhya nchini humo. Ravi Shankar Prasad Wakili wa Wahindu ambaye anashughulikia kesi hiyo amewaambia waandishi wa habari ndani ya Mahakama Kuu ya jimbo la Utta Pradesh kwamba, mahakama hiyo imeamua kuligawa eneo hilo kwa pande zote mbili ili kumaliza mgogoro ulioko kati ya Waislamu na Wahindu. Hata hivyo Mahakama Kuu ya India imeeleza kuwa, mipango ya kugawa eneo hilo utafanyika katika muda wa miezi mitatu ijayo. Eneo linalozozaniwa kati ya Waislamu na Wahindu, lilikuwa limejengwa Msikiti wa Babri, ambapo mwaka 1992 , msikiti huo uliharibiwa na Wahindu wenye kufurutu mipaka. Kuharibiwa kwa Msikiti huo kulipelekea yazuke mapigano kati ya Waislamu na Wahindu na kusababisha maelfu ya watu kupoteza maisha yao.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!