Searching...
Friday, October 1, 2010

Maandamano ya wananchi wa India wakilalamikia michezo ya madola

Sample ImageMaelfu ya wananchi wa India wameandamana mjini New Delhi kwa siku ya pili mfululizo wakitaka isusiwe michezo ya jumuiya ya madola itakayofanyika hivi karibuni nchini humo. Michezo ya jumuiya ya madola imepangwa kufunguliwa rasmi siku ya Jumamosi ijayo, mjini New Delhi. Makundi mbalimbali ya kijamii ambayo yameandaa maandamano hayo yameeleza kuwa, wananchi wa India wanahitajia mikate na ajira, na wala siyo michezo hiyo ambayo huzishirikisha nchi zilizowahi kutawaliwa na Uingereza. Hali kadhalika waandamanaji hao wa India wamelalamikia vikali matamshi ya kibaguzi yaliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Michezo ya Jumuiya ya Madola, na kuchoma moto kikatuni chake. Imeelezwa kuwa, India imegharamika zaidi ya dola bilioni tatu kwa minajili ya kuandaa michuano hiyo. Michezo ya 19 ya Jumuiya ya Madola kwa mara ya kwanza inafanyika nchini India, na ni mara ya pili kwa mashindano hayo kufanyika barani Asia. Malaysia iliwahi kuandaa michezo hiyo mwaka 1998, katika mji wa Kuala Lumpur.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!