Searching...
Thursday, September 30, 2010

Mahakama kutoa uamuzi wa umiliki wa ardhi inayogombaniwa India

 Sample ImageHali ya taharuki imetanda mjini Ayodhya kaskazini mwa India huku Mahakama Kuu ya Allahabad ikitazamiwa kutoa uamuzi wake kuhusu umiliki wa kipande cha ardhi kinachogombaniwa na jamii mbili za Waislamu na Wahindu. Habari zinasema, makumi ya maelfu ya polisi wa kupambana na ghasia wamelizingira eneo hilo ambako kunapatikana kituo cha kidini, kilichozua uhasama na migawanyiko inayoendelea kati ya jamii hizo kwa zaidi ya miaka 60 sasa. Pande mbili zimekuwa ziking'ang'ania umiliki wa kipande hicho cha ardhi na kusema kuwa, kina umuhimu kwa imani zao ikizingatiwa kuwa kiko katika eneo la kihistoria. Msikiti wa Babri ulioko katika ardhi hiyo ulibomolewa na genge la wakereketwa wa Kihindi mwaka wa 1992, likidai kuwa linataka kujenga hekalu la miungu yao ya Ram. Mahakama Kuu ilitupilia mbali rufaa iliyowasilishwa kwake na kiongozi wa zamani wa ngazi za juu wa serikali ya nchi hiyo, akitaka iakhirishe uamzui huo hadi pale Mashindano ya Kimataifa ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola yanayotarajiwa kuanza hivi karibuni yatakapomalizika. Msikiti huo wa kihistoria uliohujumiwa na genge hilo la Wahindu, ulijengwa katika karne ya 16

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!