Searching...
Tuesday, October 5, 2010

Mabaki ya sanamu la Farao yapatikana Misri.

Ahmenhotep III wa Misri
Sanamu la mfalme Ahmenhotep III wa zamani Misri ambalo mabaki yake yamegunduliwa kusini mwa nchi.
Wataalam wa mambo ya kale nchini Misri wamechimbua sehemu ya mabaki sanamu ya zaidi ya miaka elfu tatu ya mfalme wa zamani ambaye inaaminika alikuwa babu wa mfalme maarufu, Tut (Tutankhamun).
Mkuu wa maswala ya kale Misri, Zahi Hawass, anasema sanamu ya Amenhotep III (wa tatu) iligundulika mahali palipokuwa na makazi yake katika mji wa kusini wa Luxor. Hawass alisema Jumamosi mabaki hayo yanaonyesha Amenhotep akiwa amekaa katika kiti cha ufalme.
Wataalam wanaamini sanamu kamili ilikuwa na ukubwa wa karibu mita tatu.
Farao Amenhotep III alitawala ufalme wa Misri wakati wa kilele cha ustaarabu kutoka miaka ya 1390 hadi 1350 BC. Ufalme huo ulikuwa umeenea kutoka kaskazini ya Sudan ya sasa mpaka Syria.
Mjukuu wake, Mfalme Tut, alivutia macho ya dunia nzima baada ya wataalam kugundua kaburi lake likiwa limejaa vito vya thamani mwaka 1922. Mfalme huyo kijana wa chini ya miaka 20 alifariki 1324 BC.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!