Searching...
Tuesday, October 5, 2010

Mo Ibrahim yaelezea utawala bora Afrika

Mo Ibrahim, muanzilishi wa Mo Ibrahim Foundation, right, akizungumza na Kofi Annan, katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa
Utafiti mpya umebaini  kwamba wananchi wengi wa Afrika wanapata fursa kubwa za uchumi lakini wanapoteza haki za kisiasa na usalama.

Ripoti ya kielelezo cha kila mwaka cha taasisi ya Mo Ibrahim juu ya utawala bora barani Afrika imetolewa Jumatatu.  Watafiti wamegundua kwamba zaidi ya nchi 40 za Afrika zimepata mafanikio katika miaka mitano iliyopita katika maeneo mawili makuu, fursa za uchumi stahmilivu na afya na ustawi wa jamii.

Lakini watafiti wamesema mataifa 35 ya Afrika yalionesha kushuka kwa kiwango cha usalama na utawala wa kisheria. Nchi nyingine nyingi zimeshindwa katika eneo la ushiriki wa kisiasa na haki za binadamu.

Mwanzilishi wa utafiti huu mfanyabiashara wa Sudan, Mo Ibrahim alielezea matokeo kama mchanganyiko wa picha kuhusu mafanikio kuelekea utawala bora barani Afrika.

Utafiti ulitazama nchi za Mauritius, Ushelisheli, Botswana, Cape Verde na Afrika Kusini kama nchi zinazoendeshwa vizuri barani humo. Nchi tano za chini zilikuwa Eritrea, Zimbabwe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Chad na Somalia.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!