Searching...
Wednesday, July 14, 2010

Mamia waandamana Ufaransa kukosoa ukoloni mambo leo barani Afrika

Sample ImageMamia ya watu waliandamana jana mjini Paris wakiitaka Ufaransa kukomesha ukoloni mambo leo katika makoloni yake ya zamani barani Afrika. Waandamanaji hao wamelaani mwaliko uliotolewa na Rais Nicolas Sarkozy kwa viongozi wa nchi 13 za Kiafrika kwa ajili ya kushiriki kwenye sherehe za siku ya taifa ya Ufaransa zinazofanyika hii leo.
Waandamanaji hao wamesema lengo la mwaliko huo ni kutilia mkazo utiifu wa makoloni ya zamani ya Ufaransa kwa serikali ya Paris. Waandamanaji hao pia wamelaani ukoloni mambo leo unaofanywa na Ufaransa katika nchi za Afrika hususan makoloni ya zamani ya nchi hiyo.
Baadhi ya waandamanaji hao wameitaka Ufaransa na wakoloni wa zamani kuilipa fidia Afrika kutokana na kupora utajiri na maliasili za bara hilo na maafa yaliyofanywa na wakoloni hao katika nchi za bara hilo. Maandamano hayo yametayarishwa na jumuiya 80 za Kifaransa na Kiafrika na kuhudhuriwa na vyama vya upinzani

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!