Searching...
Wednesday, July 14, 2010

Uchunguzi mpya wa maoni waonyesha umaarufu wa Rais Obama unazidi kupungua

Sample ImageUchunguzi mpya wa maoni uliofanywa na gazeti mashuhuri la The Washington Post kwa ushirikiano na kanali ya televisheni ya ABC nchini Marekani umeonyesha kuwa umaarufu wa Rais Barack Obama wa nchi hiyo umepungua kwa kiwango kikubwa. Matokeo ya uchunguzi huo yanaonyesha kuwa takriban asilimia 60 ya Wamarekani hawana imani na Rais Obama hususan katika upande wa kufanya maamuzi muhimu yanayoiathiri nchi yao. Weledi wa masuala ya kisiasa wamesema kuwa kushindwa stratejia za Washington huko Afghanistan na Iraq na suala la kuvuja mafuta ya petroli katika ghuba ya Mexico ambapo Marekani hadi sasa haijafanikiwa kulitatua tatizo hilo ni miongoni mwa mambo yaliyopelekea kiongozi huyo apoteze zaidi umaarufu wake. Mwaka mmoja uliopita Rais Obama alikuwa miongoni mwa viongozi mashuhuri zaidi duniani lakini hali hiyo imekua ikibadilika kila uchao.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!