Searching...
Wednesday, July 14, 2010

Abou Gheit: Utatuzi wa mgogoro wa maji ya Mto Nile unahitaji miongo kadhaa

Sample ImageWaziri wa Mambo ya Nje wa Misri amesema kuwa utatuzi wa hitilafu zilizojitokeza kuhusu matumizi ya maji ya Mto Nile kati ya nchi za kandokando ya mto huo unahitaji miaka mingi na huenda miongo kadhaa. Ahmad Aboul Gheit amesema safari yake ya wiki iliyopita nchini Ethiopia ilikuwa na mafanikio kuhusu kadhia hiyo na kwamba mawaziri husika wa nchi za kandokando ya Mto Nile watakutana hivi karibuni katika mji mkuu wa Kenya kujadili suala hilo.
Hitilafu juu ya hisa za nchi zilizoko kandokando ya Mto Nile zilishadidi zaidi mwezi Mei mwaka huu baada ya nchi za Ethiopia, Uganda, Tanzania, Rwanda na Kenya kutia saini makubaliano mapya ya kugawana maji ya mto huo na kutupilia mbali mkataba wa zamani uliotayarishwa katika kipindi cha ukoloni. Misri na Sudan zimepinga makubaliano hayo ambayo yanapunguza hisa zao za maji ya Mto Nile

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!