Searching...
Thursday, July 1, 2010

China yasamehe ushuru wa forodha kwa bidhaa za aina nyingi zaidi kutoka nchi zilizo nyuma kabisa barani Afrika

Kwa mujibu wa makubaliano husika, kuanzia tarehe 1 Julai asilimia 6 ya bidhaa zinazoingizwa China kutoka nchi 26 za Afrika zilizo nyuma kimaendeleo zimesamehewa ushuru wa forodha.

Habari zinasema nchi hizo ni pamoja na Ethiopia, Guinea, Uganda, Sudan, Afrika ya Kati na Madagascar. Zaidi ya aina 4700 za bidhaa zimejumuishwa kwenye sera hiyo. Katika miaka mitatu ijayo, asilimia 95 ya bidhaa zinazoingizwa China kutoka nchi zote za Afrika zilizo nyuma kabisa kimaendeleo na zenye uhusiano wa kibalozi na China zitanufaika na sera hiyo.

Hivi sasa kuna nchi 30 za Afrika zilizo nyuma kimaendeleo zenye uhusiano wa kibalozi na China, mbali na nchi hizo 26, nyaraka husika za nchi 4 nyingine ambazo ni Angola, Senegal, Niger na Somalia bado zinashughulikiwa, na sera hiyo itaanza kutekelezwa mwanzoni mwa mwaka 2011.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!