Searching...
Wednesday, June 30, 2010

Sherehe ya siku ya jumba la Djibouti yafanyika kwenye maonesho ya kimataifa ya Shanghai

Sherehe ya siku ya jumba la Djibouti imeanza kufanyika asubuhi ya tarehe 30 kwenye maonesho ya kimataifa ya Shanghai. Waziri wa utalii wa Djibouti Bibi. Hasna Daoud na naibu waziri wa utamaduni wa China Bw. Wang Wenzhang wamehudhuria sherehe hiyo na kutoa hotuba.

Bibi. Hasna amesema jumba la Djibouti litaonesha mazingira ya asili na utamaduni wa jadi vyenye sifa ya kipekee, na ameyatakia mafanikio ya maonesho ya kimataifa ya mwaka 2010 ya Shanghai.

Bw. Wang anaamini kuwa Djibouti itaonesha sifa yake ya kipekee katika maonesho ya kimataifa ya Shanghai.

Kwenye sherehe hiyo, wasanii kutoka Djibouti walifanya maonesho ya nyimbo na ngoma kwa watazamaji.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!