Searching...
Monday, July 12, 2010

Milipuko haitaathiri na kuufanya mkutano wa wakuu wa AU uahirishwe

Msemaji wa serikali ya Uganda Bw. Fred Opolot tarehe 12 amesisitiza kuwa milipuko miwili iliyotokea usiku wa manane wa tarehe 11 huko Kampala haitaathiri na kuufanya mkutano wa wakuu wa Umoja wa Afrika uahirishwe kufanyika nchini humo.

Polisi nchini Uganda tarehe 12 imethibitisha kuwa milipuko hiyo miwili imesababisha vifo vya watu 64, wakiwemo wageni zaidi ya 10, na wengine 71 walijeruhiwa. Wiki moja baada ya milipuko hiyo, mkutano wa 15 wa wakuu wa Umoja wa Afrika unatarajiwa kufanyika huko Kampala, na wakuu wa nchi nyingi za Afrika watahudhuria mkutano huo, hivyo namna ya kuhakikisha usalama katika kipindi cha mkutano huo inafuatiliwa na Uganda na wajumbe wa mkutano huo.

Habari nyingine zinasema milipuko hiyo miwili ilitokea katika mkahawa wa Ethiopia ulioko mashariki mwa Kampala na klabu ya soka iliyoko kusini mwa mji huo. Wakati milipuko hiyo inatokea, mashabiki wa soka mia kadhaa walikuwa wamekusanyika katika sehemu hizo wakitazama fainali ya kombe la dunia.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!