Searching...
Tuesday, June 8, 2010

UM waongeza juhudi kupunguza vifo kwa wajawazito kutekeleza malengo ya milenia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo ametoa wito wa kufanyika juhudi za pamoja za kukomesha kile alichokiita kashfa ya vifo vya wanawake wengi wakati wa kujifungua.

Ban Ki-moon-Washington

Ban Ki-moon-Washington

Amesema hata taratibu ambazo ni za kawaida kabisa kama usafi wa wodi za wazazi na kuwepo kwa wakunga wakati wanapohitajika kutasaidia sana kupunguza vifo vingi vya wakati wa kujifungua. Ameongeza kuwa mambo mengine kama kupimwa damu, kuonana na madaktari ambao ni wataalamu, na kupata msaada wakati wa kujifungua kunaweza kuleta tofauti kubwa sana.

Ban ameyasema hayo katika mkutano wa kimataifa mjini Washington wenye lengo la kutafuta suluhu ya matatizo yanayoathiri wanawake na wasichana duniani kote.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!