Searching...
Tuesday, June 8, 2010

Abuja-Mkutano wa ECOWAS kuhusu usalama na usuluhishi wa mgogoro wafanyika nchini Nigeria

Mkutano wa 27 wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi ECOWAS kuhusu usalama na usuluhishi wa mgogoro unaendelea kufanyika huko Abuja, Nigeria.

Kwenye mkutano huo wa siku 2 mwenyekiti wa kamati ya ECOWAS Bw. James Victor Gbeho amesema, eneo la Afrika magharibi liko kwenye kipindi muhimu cha kubadilika kwa serikali za nchi, ambapo hali ya usalama wa eneo hilo inakabiliwa na changamoto nyingi, kwa hiyo mkutano huo utazihimiza Niger, Guinea, Guinea Bissau na Togo zitulize migogoro yao, na kuihimiza Cote d'Ivoire ifanye uchaguzi mkuu, ambao umeahirishwa mara nyingi.

Kwenye mkutano huo mjumbe maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kwenye eneo la Afrika magharibi Bw. Said Djinnit amesema, Umoja wa Mataifa utaimarisha ushirikiano kati yake na ECOWAS, na kuhimiza amani ya kudumu na maendeleo katika eneo la Afrika magharibi.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!