Searching...
Monday, June 28, 2010

Uingereza ndilo soko kuu la madawa ya kulevya barani Ulaya

Sample ImageOfisi ya kupambana na madawa ya kulevya na jinai ya Umoja wa Mataifa imetangaza kuwa, Uingereza imebadilika na kuwa soko kuu la madawa ya kulevya aina ya kokeini kati ya nchi za Ulaya. Taarifa ya ofisi hiyo ya Umoja wa Mataifa imeeleza kuwa, Uingereza inahesabiwa kuwa soko kuu la kuuza na kununua madawa hayo ya kulevya, ikizitangulia nchi za Uhispania, Italia, Ujerumani na Ufaransa. Taarifa hiyo imeongeza kuwa matumizi ya madawa ya kulevya katika nchi za Uingereza na Uhispania ni makubwa zaidi kuliko Marekani. Taarifa hiyo imeongeza kuwa, matumizi ya madawa ya kulevya nchini Uingereza na nchi nyingine ndogo huko Ulaya inazidi kuongezeka, lakini Amerika ya Kaskazini inaongoza kwa kuwa soko la matumizi ya mihadarati duniani kwa kufikia matumizi ya kiwango cha asilimia 40 duniani. Wataalamu wa mambo wanaeleza kuwa, baada ya vikosi vya kigeni kulitokomeza kundi la Taleban na al Qaeda nchini Afghanistan mwaka 2001, uzalishaji wa mihadarati nchini humo umeongezeka kwa asilimia 40, ikilinganishwa na hapo kabla. Hivi karibuni Rais Hamid Karzai wa Afghanistan amesema kuwa, mihadarati imekuwa doa jeusi ambapo faida ya mabilioni ya dola inaingia kwenye mifuko ya wageni na jina baya linaendelea kubaki kwa wananchi wa Afghanistan.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!