Searching...
Monday, June 28, 2010

Sudan na Misri zasema hazitatia saini mkataba mpya wa Mto Nile

Sample ImageMisri na Sudan zimesema hazitakubali kulazimishwa kutia saini mkataba mpya wa kugawana maji ya Mto Nile.
Mawaziri wa maji wa nchi hizo mbili ambazo ndio watumiaji wakubwa zaidi wa maji ya Mto Nile wametoa matamshi hayo huko Addis Ababa Ethiopia katika mazungumzo kuhusu ugawanaji maji ya mto huo ambao unaaminika kuwa mrefu zaidi duniani.
Ethiopia, Kenya, Rwanda, Tanzania na Uganda zilitia saini makubaliano mwezi Machi ambayo yanachukua mahala pa ule mkataba wa mwaka 1929 wa zama za ukoloni kati ya Misri na Uingereza ambao uliipa Misri turufu ya kuamua kuhusu miradi yote ya Mto Nile na vyanzo vyake. Misri na Sudan zinasisitiza kuwa zitaendelea kuwa na haki ya kutumia asilimia kubwa ya maji ya Nile.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!